Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Dalili ya wazi na kubwa Kuhusu Kupigana kwa Malaika Pembeni ya Ali (as).
2496 - Imam Hasan (a.s) alisema:
"Mtume (saww) alikuwa akimtuma (Ali) kwenye vita akiwa na bendera, naye hakuwa anarudi mpaka Mwenyezi Mungu amemfungulia ushindi, Jibril (as) akiwa upande wa kulia wake, na Mikail (as) upande wa kushoto wake." - yaani: Ali (r.a).
Imepokelewa katika "Silsilat al-Ahadith al-Sahihah" (Juzuu ya 5, uk. 660) na Sheikh Al-Albani amesema: Hadithi hii ni Hasan (nzuri).
_
الدليل العلي في قتال الملائكة بين يدي علي
2496 - قال الإمام الحسن عليه السلام:《كان يبعثه البعث فيعطيه الراية، فما يرجع حتى يفتح الله عليه جبريل عن يمينه، وميكائيل عن يساره》 - يعني عليا رضي الله عنه-
《سلسلة الأحاديث الصحيحة ٦٦٠/٥ قال الألباني: حسن.
_
Basi, kwa Hakika Amirul-Mu'minin Ali (a.s) hakuwa anarudi kutoka vitani mpaka apate ushindi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Na ni fadhila iliyo kubwa kiasi gani kuwa Malaika Jibril (as) anapigana upande wa kulia wake, na Mikail (as) upande wa kushoto wake.
Na mtu wa namna hiyo ndiye anayestahiki zaidi kuwa mfano halisi wa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wale walio pamoja naye ni wakali juu ya makafiri, ni wenye kuhurumiana wao kwa wao." — [Surat Al-Fath, Aya ya 29].
_
فأمير المؤمنين (ع) لا يرجع من القتال حتى يفتح الله عليه. وما أعظمها من فضيلة أن جبريل يقاتل عن يمينه وميكائيل عن يساره.
ومن كان كذلك كان أكبر مصداق لقوله تعالى:
{مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ}.
(الفتح ٢٩).
Your Comment